Kenyan mugged in Offenbach – Culprit arrested and charged

Asubuhi ya kuamkia Jumapili, Mkenya mmoja anayeishi Offenbach alijipata ameporwa mali mali hakuripoti kwenye kituo cha polisi wala kueleza yeyote.

Polisi walipata repoti baada ya masaa mawili kuhusu kikundi cha barobaro waliofanana kama waliotoka Europa Mashariki, walioonekana katika barabara ya Groß-Hasenbach. Vijana wale walipowaona polisi wote walihepa isipokuwa mmoja aliyekuwa anajaribu kutoa makaratasi toka kijipochi alichokibeba. Kwa harakati za kutoa makaratasi yale na kujaribu kukimbia alijipata amekamatwa na polisi.

Makaratasi yale yalipatikana kuwa vitambulisho na vyeti, vilivyokuwa sio vya kijana aliyekamatwa. Polisi kumpigia simu mwenye vyeti walipata ni kijana mmoja anayeishi Ujerumani Mashariki. Kijana huyu aliweza kuwaelezea polisi kuwa alikuwa ameporwa mali lakini kwa utatanishi wa lugha, hakuweza kueleza hususan wapi kitendo hicho kilitendeka wala alikoishi wakati wa kitendo hicho kutendeka.

Kwa bahati nzuri palitokea raia mwema aliyeweza kuwaeleza polisi jinsi mshukiwa huyo alionekana akimwibia Mkenya fulani papo hapo alipopatwa na polisi. Mkenya yule wa miaka kumi na saba, alishikwa na mshukiwa yule saa sita unusu usiku wa kuamkia Jumapili. Mshukiwa huyo alimshika Mkenya huyo akamrusha kwenye sakafu na kumwibia kipochi.

Polisi walipomkabili mshukiwa huyo na kisa hicho walivyoelezwa na raia, mshukiwa aliweza kuwapa kipochi alichokuwa amememwibia Mkenya huyo. Polisi walimkamata na kwenda naye kwenye kituo cha polisi alikoshukiwa na mashtaka ya wizi barabarani. Mkenya yule bado hajapatikana ilikupeana ushuhuda wake wala kumshtaki mshukiwa huyo kwa kumwibia wala kumshambulia.

Haya in English:

A Kenyan was mugged in Offenbach on Sunday morning at half past midnight but he never reported. 2hrs later the police were alerted of a group of young boys hanging around along the Graß-Hasenbach street in Offenbach. On spoting the police the group split but one of the boys was busy trying to throw away papers he was removing from the wallet he was holding. The polic caught up with him and found that the papers he was throwing didn’t belong to him but were identification papers of a guy in East Germany. They called the owner of the papers but due to language issues they couldn’t figure out where he currently resides nor where exactly he’d been mugged.
One of the loyal citizens approached the police and informed them of the mugging involving the Kenyan that had happened Sunday morning. The suspect on being confronted with the story, he produced the wallet belonging to the Kenyan. He was taken to the police station and charged with stealing on the streets but because the Kenyan couldn’t be reached the suspect walked free.

Share with friends: